Coastal Union leo imetumia vyema uwanja wa Mkwakwani ikipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Bao pekee la Coastal Union lilifungwa na kiungo Gustava Saimon
Ushindi huo umeiondoa Coastal Union katika eneo la play-off hadi nafasi ya 10 baada ya kufikisha alama 30
Presha inazidi kuongezeka upande wa Mtibwa Sugar wakiwa na alama 29 alama mbili juu ya play-off wakishuka hadi nafasi ya 11
Nayo Mbeya City imeendelea kubaki eneo la play-off baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar
Ally Nassor Idd alifunga bao pekee la Kagera Sugar ambao walicheza takribani dakika 45 wakiwa pungufu