Paris St-Germain wanafikiria kumuuza Neymar msimu huu wa joto - huku Chelsea na angalau klabu nyingine moja ya Premier League ikitafakari kumnunua mshambuliaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 31 (Mirror)
Mshambulizi wa PSG Lionel Messi anataka kurejea Barcelona lakini klabu hiyo ya Uhispania inahitaji kuongeza pauni milioni 88 kupitia mauzo ya wachezaji na kuamsha 'kichocheo kingine cha kiuchumi' ili kumsajili tena nahodha huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 35 (Mail)
Mshambulizi wa Tottenham Harry Kane yuko kwenye orodha ya wanaolengwa na Bayern Munich msimu huu wa joto, ingawa nahodha huyo wa England mwenye umri wa miaka 29 anaaminika kusita kuondoka Ligi ya Premia (Bild - in German)
Juventus wanapanga kumnunua mlinzi wa Senegal Kalidou Koulibaly, 31, ambayehajafurahia hali yake baada ya msimu mmoja tu akiwa Chelsea . (Gazzetta dello Sport - in Italian)
Liverpool wamepunguza hamu yao ya kumnunua mlinzi wa Croatia mwenye umri wa miaka 21 Josko Gvardiol kwani wanaamini kwamba thamani ya Red Bull Leipzig ya £80m kwa mchezaji huyo ni kubwa mno.. (Football Insider)
Manchester City wanapanga kumnunua beki wa pembeni wa Brentford kutoka Scotland Aaron Hickey, 20, ambaye thamani yake ni pauni milioni 30.. (Sun)
Kocha wa zamani wa Uhispania Luis Enrique hayupo tena kwenye kinyang'anyiro cha kuwa meneja mpya wa Chelsea (Fabrizio Romano) Wachezaji wa Chelsea wamefurahishwa na uwezekano wa kocha wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino kuwa meneja wao mpya. (Telegraph - usajili unahitajika)
Arsenal, Chelsea na Liverpool zimeonesha nia ya kutaka kumnunua beki wa Valencia Yunus Musah mwenye umri wa miaka 20 kutoka Marekani. (90Min)
Chelsea hawana nia ya kumuuza mlinzi wa England aliye chini ya umri wa miaka 21 Levi Colwill, 20, msimu huu wa joto licha ya Liverpool , Tottenham na Manchester City kumtaka (Football Insider)
Mshambulizi wa zamani wa Liverpool na Uingereza Robbie Fowler anafikiria kutuma ombi la kuajiriwa kama meneja katika klabu ya Ligi ya Pili ya Tranmere Rovers (Sun)
Newcastle, Crystal Palace na Brighton wanamfuatilia kiungo wa kati wa Blackburn anayesifiwa sana kwa ubora wa mchezo wake mwenye umri wa miaka 18 Adam Wharton (Sun)
BBC