Tanzania Prisons imekuwa timu ya kwanza kupata ushindi kwenye uwanja wa Nyankumbu huko Geita wakiwachapa wenyeji wao Geita Gold mabao 3-1 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Ni matokeo muhimu kwa Tanzania Prisons ambayo yanazidi kuwaweka salama katika kujinusuru kuteremka daraja
Prisons imefikisha alama 31 na kusogea mpaka nafasi ya tisa katika msimamo wa ligi
