Azam Fc wanaitaka nafasi ya tatu Ligi Kuu

Joel JJ By Joel JJ
β€’
25 Apr 2023
Azam Fc wanaitaka nafasi ya tatu Ligi Kuu

Nyota wa Azam FC, Ayub Lyanga amesema mabao mawili aliyofunga kwenye ushindi wa 3-1 dhidi ya Ruvu Shooting yameongeza chachu ya ushindani kwenye kikosi chao ambacho amekiri kuwa kinahitaji nafasi ya tatu kwenye msimamo

Ushindi walioupata Azam FC umewafanya wapande nafasi moja kutoka nne hadi tatu baada ya kukusanya pointi 53, wakiwashusha Singida Big Stars ambao wapo nyuma kwa mchezo mmoja wakiwa na 51 na Ruvu Shooting wameshuka hadi nafasi ya mwisho

Lyanga amesema ni matokeo mazuri kwao na anafurahi kuwa miongoni mwa wachezaji walioipa matokeo ya ushindi timu yake ambayo ameweka wazi kuwa pamoja na kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi kimataifa bado wanaitaka nafasi ya tatu

"Ushindi tulioupata ugenini dhidi ya Ruvu Shooting unaturudisha imara nyumbani tukiwasubiri Namungo tutaingia mchezoni tukiwa kwenye hali nzuri ya ushindani"

"Nimefunga mabao mawili siyo kwa juhudi zangu ni namna timu ilivyocheza kwa kushirikiana na kuelewana tutaendelea tulipoishia ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kupata matokeo nyumbani dhidi ya Namungo tukijiandaa na Simba hatua ya nusu fainali FA," alisema Lyanga

ADVERTISE HERE

More Stories

Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
2h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
4h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
5h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
5h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
7h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
7h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
7h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
20h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
1d ago
READ MORE β†’