Azam - Local

Azam Fc yaunga mkono vita ukatili wa kijinsia

Joel JJ By Joel JJ
β€’
26 Apr 2023
Azam Fc yaunga mkono vita ukatili wa kijinsia

Azam FC imeungana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum katika kupiga vita ukatili wa kijinsia na watoto

Katika kuliwekea uzito jambo hilo, Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, alikutana na uongozi wa timu hiyo, Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat' na Makamu Mwenyekiti, Omary Kuwe na kujadili kwa kina watakavyoshirikiana kupinga ukatili huo.

Wizara hiyo, ipo katika kampeni kubwa ya kutokomeza ukatili huo, ambapo imeandaa Tamasha kubwa la Zijue Fursa, Imarisha Uchumi, Kataa Ukatili (ZIFIUKUKI) litakalofanyika kwenye Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam kuanzia Ijumaa hii Aprili 27 hadi 29 mwaka huu.

Dkt. Gwajima, amesema kuwa mbali na tamasha hilo kushirkisha michezo, pia litakuwa na fursa mbalimbali za uwezeshaji kiuchumi katika jamii, kama ilivyo sera ya Rais wa Serikali ya Awamu ya Sita, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan

"Tamasha hili limebeba taswira nzima ya kampeni ya serikali kupitia Wizara wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum iliyozinduliwa mwaka 2017-2018 inayosema twende pamoja, Tanzania sasa, Ukatili basi," alisema

Naye Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat', aliishukuru Serikali kwa kuwachagua kuwa miongoni mwa mabalozi wake katika kampeni hiyo na kuahidi kuwa watashiriki kikamilifu kupinga ukatili wa kijinsia na watoto. Tukutane Leaders Ijumaa hii! Tukachangamkie fursa za kiuchumi na kupinga ukatili wa kijinsia na watoto.

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
1h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
1h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
2h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
5h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
9h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
9h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
10h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
11h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
12h ago
READ MORE β†’