Baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya wapinzani wao wa mbio za ubingwa Arsenal, mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola amesema kuwa kikosi chake kimethibitisha kuwa kinaweza kufanikisha malengo pale wanapohitaji ushindi
Kikosi cha Guardiola kiliwashinda viongozi Arsenal 4-1 kwenye Uwanja wa Etihad, na sasa wako nyuma kwa pointi mbili wakiwa na michezo miwili ya ziada
City wamebakisha mechi saba, wakianza na safari ya Jumapili dhidi ya Fulham kabla ya mechi za nyumbani dhidi ya West Ham na Leeds
"Hatuwezi kupoteza umakini wetu. Sasa iko mikononi mwetu," alisema Guardiola
Mabao ya Manchester City katika mchezo huo yalifungwa na Kelvin De Bruyne aliyefunga mawili, John Stones na Haaland aliyefikisha mabao 33 ya ligi
Haaland anahitaji kufunga bao moja tu kuifikia rekodi ya muda wote ya mabao katika msimu mmoja kwenye ligi inayoshikiliwa na Alan Shearer (mabao 34)