Yanga - Local

Yanga yamuahidi Rais Samia fainali Shirikisho

Joel JJ By Joel JJ
27 Apr 2023
Yanga yamuahidi Rais Samia fainali Shirikisho

Klabu ya Yanga imemuahidi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk Samia Suluhu Hassan kuwa wataendelea kupambana katika michuano ya kimataifa na ikiwezekana kufika hadi fainali kwa lengo la kuitangaza Tanzania

Hayo yalisemwa jana na Afisa Habari wa klabu hiyo, Ally Kamwe wakati akikabidhiwa kitita cha Sh Milioni 10 zilizotokana na ushindi wa mabao 2-0 ugenini katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya robo fainali waKombe la Shirikisho dhidi ya Rivers United ya Nigeria

"Tuna mshukuru Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza ahadi ake kwa vitendo tumepokea pesa hizi na kiukweli zimetupa hamasa kubwa hadi kufika hapa sisi Yanga tunamuahidi kuipeperusha bendera ya nchi hii kwa kufika mbali ikiwezekana kubeba ubingwa wa Kombe la Shirikisho," alisema Kamwe

Yanga Jumapili hii itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kurudiana na Rivers United na inahitaji sare au ushindi wowote ili kuandika historia ya kutinga Nusu Fainali ya michuano hiyo kwa timu za Tanzania

Katika hatua nyingine, Kamwe amewataka mashabiki wa Yanga kununua tiketi kwa wingi kuhakikisha wanaujaza uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumapili katika mchezo wao dhidi ya Rivers United

Kamwe amesema ni nafasi adimu kwa mashabiki wa soka nchini kushuhudia historia ya aina yake ikiandikwa na klabu yao hivyo wanapaswa kwenda uwanjani kuwa sehemu ya kumbukumbu hiyo itakayodumu kwa miaka mingi

More Stories

BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
15m ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
29m ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
1h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
1h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
1h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
1h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
2h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
4h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
14h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
14h ago
READ MORE →