Mbeya City yaapa kupambana kubaki Ligi Kuu

Joel JJ By Joel JJ • 27th April 2023


Mbeya City yaapa kupambana kubaki Ligi Kuu

Licha ya kupoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Kagera Sugar, Mbeya City imepania kupambana ili kuhakikisha wanabaki ligi kuu

 Timu hiyo imekusanya pointi 27 baada ya kucheza mechi 27 ipo kwenye hatari ya kushuka daraja

Kocha Msaidizi wa Mbeya City, Anthony Mwamlima amesema kuwa bado wana mechi za kucheza na watafanyia kazi makosa ambayo yametokea.

"Kweli matokeo ambayo tunapata sio mazuri lakini bado hatujakata tamaa kwa kuwa kuna mechi za kucheza hizo tatu zilizobaki tukipambana tukipata matokeo tutaondoka hapa tulipo"

“Hakuna ambaye anapenda kuona hatushindi ila ni mpira na haya ni matokeo kwenye uwanja wa mazoezi tunakwenda kufanyia kazi makosa, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi," alisema


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.