Simba matumaini kibao ikiikabili Wydad leo

Joel JJ By Joel JJ
β€’
28 Apr 2023
Simba matumaini kibao ikiikabili Wydad leo

Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira amesema wamejiandaa kuwashangaza Wydad Athletic katika mchezo wa mkondo wa pili robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Leo Simba itakuwa ugenini katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Mohammed V, saa 4 usiku kwa saa za Tanzania

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari jana, Robertinho alisema amekiandaa kikosi chake kimbinu kukabiliana na Wydad katika mchezo muhimu wa kuwania tiketi ya kutinga nusu fainali

"Tutawashangaza wapinzani wetu kwa sababu tumefanya kazi kubwa kufika hapa tulipo, tumekuwa tukibadili mazoezi kulingana na mpinzani tunayekutana nae"

"Binafsi ningependa tushinde magoli mawili au matatu lakini hata goli moja litatufaa kutokana na kile tulichokipata kwenye mchezo wa kwanza"

"Nina imani kubwa na wachezaji wangu na viongozi kwa ujumla, tumejiandaa kikamilifu kuelekea mchezo huu. Tumekuwa na mfululizo wa matokeo mazuri, hili ni jambo muhimu kwetu," alisema Robertinho

Nae kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho alisema hawana hofu yoyote kuelekea mchezo huo, wamefanya maandalizi kabamba kuhakikisha wanashinda

Sakho amesema hawana hofu na mashabiki wa Wydad zaidi vurugu zao zitawaongezea ari ya kupambana

Simba leo inahitaji ushindi au matokeo yoyote ya sare ili kutinga nusu fainali ya michuano hiyo

ADVERTISE HERE

More Stories

Tunakwenda kucheza na timu mzito na ngumu: Juma Mgunda
Tunakwenda kucheza na timu mzito na ngumu: Juma Mgunda
11m ago
READ MORE β†’
Jack Grealish aingia matatani Everton baada ya kuripotiwa kula bata siku mbili mfululizo
Jack Grealish aingia matatani Everton baada ya kuripotiwa kula bata siku mbili mfululizo
23m ago
READ MORE β†’
NBC Premier League: Mechi mbili za kibabe kupigwa leo.
NBC Premier League: Mechi mbili za kibabe kupigwa leo.
1h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya mechi kubwa inaendelea: Liverpool vs Arsenal na Napoli vs Juventus
Wikiendi ya mechi kubwa inaendelea: Liverpool vs Arsenal na Napoli vs Juventus
2h ago
READ MORE β†’
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
15h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
17h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
17h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
18h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
18h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
19h ago
READ MORE β†’