Simba - Yanga - Local

Rais Samia aongeza bonasi Simba, Yanga

Joel JJ By Joel JJ
β€’
28 Apr 2023
Rais Samia aongeza bonasi Simba, Yanga

Rais Samia Suluhu Hassan ameongeza fedha za motisha kwa timu za Simba na Yanga kutoka Sh milioni 5 hadi Sh milioni 10.

Rais atatoa fedha hizo endapo timu hizo zitafuzu kucheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na Kombe la Shirikisho.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa leo Aprili 28, 2023 amesema magoli yatakayolipiwa shilingi milioni 10 ni yale yatakayofungwa katika dakika 90 za mchezo au dakika 120 na sio magoli ya penalti.

Amesema, Rais Samia anazitakia kila la heri Simba na Yanga na amewataka wachezaji kujituma uwanjani na kutumia maarifa yao yote kuhakikisha wanashinda michezo ya kukamilisha hatua ya robo fainali ili wafanikiwe kuingia nusu fainali, ambapo kila goli litakuwa shilingi milioni 10.

Simba inacheza mchezo wa marudiano leo Aprili 28, 2023 saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki dhidi ya Wydad Casablanca nchini Morocco, wakati Yanga watawakaribisha Rivers United ya Nigeria katika mchezo wa marudiano utakaofanyika kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

Simba inacheza mchezo wa marudiano ikiwa na mtaji wa ushindi wa 1-0 ilioupata katika mchezo wa kwanza wa robo fainali uliofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam wakati Yanga itacheza mchezo wa marudiano ikiwa na mtaji wa ushindi wa 2-0 ilioupata ugenini huko nchini Nigeria.

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
5h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
5h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
5h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
9h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
12h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
13h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
13h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
14h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
15h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
16h ago
READ MORE β†’