Mkufunzi wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema wamejipanga kuhakikisha wanashinda mchezo wa kesho ili kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF
Akizungumza na wanahabari leo Aprili 29, 2023 kocha huyo amesema pamoja na ushindi walioupata ugenini wiki iliyopita lakini wanapaswa kuwa makini katika mchezo huo ili kutimiza malengo yao
"Nimezungumza na wachezaji wangu kuhusu mchezo wa kesho dhidi ya Rivers United na nimewaeleza kuwa ushindi tulioupata Nigeria utakuwa hauna maana kama tutapoteza mchezo wa kesho tunapaswa kucheza kwa kujituma kama vile tulipoteza mchezo wa kwanza," alisema Nabi
Katika mchezo huo Yanga inahitaji ushindi ay sare tu ili kuweka rekodi yakuwa timu ya kwanza Tanzania kufika hatua hiyo kwenye michuano ya Caf