Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga wamefanikiwa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Rivers United katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Yanga imetinga nusu fainali kwa matokeo ya ushindi wa jumla wa mabao 2-0 waliopata kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Nigeria
Yanga inaweka historia ya kuwa klabu ya kwanza Tanzania kutinga nusu fainali ya mashindano ya klabu yanayoandaliwa na CAF
Sasa watachuana na Malumo Galants ya Afrika Kusini mchezo wa kwanza ukitarajiwa kupigwa jijini Dar es salaam na marudiano kupigwa Afrika Kusini
Kwa hakika ni ushindi wa heshima kwa Tanzania na ligi kuu ya NBC!