Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu May 1 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
1 May 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu May 1 2023

Manchester City wanajiandaa kufanya mazungumzo na mshambuliaji wa Norway Erling Haaland, 22, kuhusu mkataba mpya. (Football Insider)

Mshambulizi wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha anahusudiwa na vilabu vya Arsenal, Juventus, Chelsea na Barcelona huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 akitarajiwa kuondoka Selhurst Park mwishoni mwa msimu mkataba wake unapomalizika. (Telegraph)

Chelsea ina imani kuwa kiungo wake wa kati wa England Mason Mount, 24, atazikataa Bayern Munich na Liverpool na kusaini mkataba mpya kusalia katika klabu hiyo. (Football Insider)

Mshambuliaji wa Juventus Dusan Vlahovic, 23, anataka kuuzwa kwenda Arsenal na Bayern Munich huku muda wa Mserbia huyo katika klabu hiyo ya Italia unaonekana umefikia mwisho (Tutto Mercato Web)

Chelsea ni miongoni mwa klabu kadhaa za Ligi kuu England zinazomfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa kati Stevenage, 16, Makise Evans. (Sun)

Newcastle United wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Roma mwenye umri wa miaka 29 kutoka Argentina Paulo Dybala. (Calcio Mercato)

Manchester United inataka kumsajili beki wa pembeni wa Paris St-Germain, Mmoroccofull Achraf Hakimi, 24. (Football Insider)

Sheffield United iko tayari kumuongezea mkataba mshambuliaji wa Scotland Oli McBurnie mwenye umri wa miaka 26 baada ya kufanikiwa kupanda daraja kucheza Ligi kuu England msimu ujao. (Sun)

Chelsea inahusishwa na mshambuliaji wa Bayern Munich na Senegal Sadio Mane, 31, ambaye alijiunga na timu hiyo ya Ujerumani akitokea Liverpool msimu uliopita wa joto. (Football London)

Klabu ya Saudi Pro League Al Nassr inamfuatilia beki wa kushoto wa Brazil Alex Telles, 30, ambaye yuko kwa mkopo Sevilla akitokea Manchester United na huenda akaungana tena na mchezaji mwenzake wa zamani wa Mashetani Wekundu Cristiano Ronaldo. (AS)

BBC

More Stories

Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
3h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
6h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
7h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
7h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
8h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
9h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
10h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
10h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
23h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
23h ago
READ MORE β†’