Kocha wa Al-Hilal Sc Florent Ibenge amelazimika kuondoka Sudan ili kukwepa machafuko yanayoendelea kutokana na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
Kupitia Ubalozi wa Ufaransa, Florent Ibenge pamoja na familia yake walibahatika kupata nafasi kwenye msafara wa kwanza uliowahamisha raia wa kigeni kutoka Sudan.
Akizungumza na Shirika la habari la BBC, kocha huyo amesema;
"bado tuna wasiwasi hasa tukiwafikiria wengine wengi tuliowaacha Sudan, nawaza sana kuhusu wachezaji wangu,ninaongea nao kila siku"
"Wachezaji wote ambao sio raia wa Sudan wameshaondoka na sasa wanaelekea Misri.Wakifika nitawafuata, pamoja na wasaidizi wangu tutaweka kambi Cairo"
"Wachezaji ambao ni raia wa Sudan wanaweza kuamua kubaki kwao, ikibidi nitabadili muundo wa timu na wachezaji" alieleza Ibenge