Baada ya kufanikiwa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika, kikosi cha Yanga hakina muda wa kupoteza kwani bado wana kazi kutetea mataji ya ndani waliyoshinda msimu uliopita
Yanga imeondoka leo kuelekea mkoani Singida kwa ajili ya mechi mbili dhidi ya Singida Big Stars
Alhamisi May 04 Yanga itashuka uwanja wa Liti kumenyana na Singida BS katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
May 07 Yanga itashuka tena uwanja wa Liti kumenyana na Singida BS katika mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
May 10 Wananchi watakuwa wamerejea Dar ambapo watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza nusu fainali ya kombe la Shirikisho dhidi ya Malumo Galants



