Leeds United wanafikiria kumteua kocha wa zamani wa West Ham na Everton Sam Allardyce, ambaye amewahi kuiona England mara moja, ili kumrithi Javi Gracia kama meneja wa klabu hiyo. (Athletic)
Kocha wa Arsenal Mikel Arteta anataka kufanya mazungumzo na kiungo wa kati wa West Ham Muingereza Declan Rice, 24, punde tu msimu unapomalizika. (Mirror)
The Gunners pia wanafikiria kumnunua mlinzi wa Crystal Palace Muingereza Marc Guehi, 22. (Mail)
Chelsea inakaribia kumpa mikoba kocha wa zamani wa Tottenham na Paris St-Germain Mauricio Pochettino kuwa meneja wa kudumu wa klabu hiyo. (90Min)
Jitihada za Sir Jim Ratcliffe za kutaka kuwa na hisa nyingi katika klabu ya Manchester United ni pamoja na kutaka udhibiti wa haraka wa masuala ya uhamisho iwapo mkataba utafikiwa. (Telegraph)
Manchester United ilituma wasaka vipaji kumtazama mshambuliaji wa Roma Tammy Abraham, 25, mwishoni mwa wiki iliyopita huku klabu hiyo ikifikiria mbadala wa mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 29. (Mirror)
Hata hivyo, Aston Villa wana uhakika wanaweza kumsajili mchezaji wa kimataifa wa England Abraham kutoka Roma - licha ya vilabu kadhaa vikubwa Ulaya kumuwinda nyota huyo. (90Min)
Aston Villa imeanza mazungumzo na mshambuliaji wa England Ollie Watkins kuhusu kuongeza mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 na klabu hiyo. (Athletic)
Tottenham na Newcastle United ni miongoni mwa vilabu vinavyosubiri kuona bei ambayo Southampton itaweka kwa ajili ya kiungo wa kati wa England James Ward-Prowse, 28, iwapo timumhiyo itashuka daraja. (Mirror)
Manchester City haitamnyima kiungo wa kati wa Ureno Bernardo Silva, 28, ruksa ya kuondoka katika klabu hiyo iwapo ataamua hivyo msimu wa joto. (90Min)
Meneja wa Crystal Palace Roy Hodgson anaamini mwenyekiti wa Eagles hao, Steve Parish anapaswa kuwa na wasiwasi kuhusu klabu kadhaa kumtaka winga Mfaransa Michael Olise, 21, msimu huu wa joto. (Evening Standard)
BBC