Namungo - Simba - Local

Namungo yapania kufuta uteja mbele ya Simba

Joel JJ By Joel JJ
β€’
2 May 2023
Namungo yapania kufuta uteja mbele ya Simba

Kocha Mkuu wa Namungo, Denis Kitambi amesema huu ni wakati sahihi kwao wa kuweza kufuta uteja mbele ya Simba wakati timu hizo zitakapokutana katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, Jumatano hii

Timu hizo zinakutana katika mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi huku Namungo ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mechi ya kwanza kwa bao 1-0, Novemba 16 mwaka jana.

Kitambi amesema licha ya ugumu wa mchezo huo ila ni muda wa kuondoa unyonge mbele ya wapinzani wao kutokana na kutokuwa na matokeo mazuri kila wakati wanapokutana

"Awali malengo yetu yalikuwa ni kumaliza nafasi nne za juu lakini ukiangalia kasi ya washindani wetu na kutokuwa na matokeo mazuri imeturudisha nyuma hivyo angalau tumalize ya tano," alisema

Kitambi aliongeza katika michezo yote iliyobaki wameanza kampeni ya kuhakikisha kila mpinzani atakayefika uwanjani mwao anakutana na wakati mgumu wa kupata ushindi ili kutimiza malengo yao

Wakati Kitambi akizungumza hayo ila timu hiyo imekuwa wanyonge kwa Simba kila inapokutana nao kwani tangu imepanda rasmi Ligi Kuu Bara msimu wa 2019/2020 haijawahi kushinda zaidi ya sare tu

Katika michezo saba ya Ligi Kuu Bara ambayo Namungo imecheza na Simba tangu msimu huo imepoteza mitano na kupata sare miwili tu na imefungwa jumla ya mabao 14 huku wao wakifunga matano tu

Mchezo huu ambao utapigwa Mei 3 unarudisha kumbukumbu ya mechi baina ya timu hizi uliopigwa pia Mei 3, mwaka jana wakati miamba hii ilipokutana kwenye Uwanja wa Ilulu na kufungana mabao 2-2

Mwanaspoti

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
7h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
7h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
7h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
11h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
14h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
15h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
15h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
16h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
17h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
18h ago
READ MORE β†’