Picha iliyopigwa baada ya mechi kati ya Liverpool dhidi ya Tottenham Hotspurs katika uwanja wa Anfield, imeonyesha Diogo Jota akiomba msamaha kwa Oliver Skipp baada ya Liverpool kushinda 4-3 dhidi ya Tottenham.
Fowadi huyo wa The Reds alimfanyia rafu mbaya Skipp tukio ambalo liliibua mjadala baada ya Jota kuonyeshwa kadi ya njano wengi wakiamini alistahili kuonyeshwa kadi nyekundu
Skipp alimwaga damu baada ya changamoto hiyo, huku bosi wa muda wa Spurs Ryan Mason akiwa na hasira kwamba Jota hakutolewa nje kwa kadi nyekundu
Nyota huyo wa Liverpool alifunga bao la ushindi dakika za lala salama, licha ya Richarlison kufunga bao la kusawazisha hapo awali



