Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 35, ataondoka Paris St-Germain mwishoni mwa msimu huu baada ya mabingwa hao wa Ufaransa kuamua kutoongeza mkataba wake. (FootMercato)
Manchester United wameainisha nyota wa tatu mbadala wa mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 29 - Mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa wa Eintracht Frankfurt Randal Kolo Muani, 24, mshambuliaji wa Roma na England Tammy Abraham, 25, na mchezaji wa kimataifa wa Argentina anayechezea Inter Milan Lautaro Martinez, 25. (FourFourTwo)
Mazungumzo ya Tottenham na meneja wa zamani wa Bayern Munich Julian Nagelsmann kuhusu kuwa meneja wao mpya yamekwama kwa sababu ya sintofahamu kuhusu nafasi ya mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo. (Telegraph)
Sam Allardyce yuko kwenye mazungumzo ya kuwa meneja ajaye wa Leeds United na amepewa bonasi ya pauni milioni 1 ikiwa ataibakisha klabu hiyo ya Elland Road kwenye Ligi kuu England. (Star)
Allardyce atapata bonasi ya zaidi ya £2.5m ikiwa ataweza kuibakisha ligi kuu Leeds United na anamtaka meneja wa zamani wa Oxford United Karl Robinson kuwa msaidizi wake pale Elland Road. (Times)
Wamiliki wenza wa Chelsea Todd Boehly na Behdad Eghbali walikutana Los Angeles mwishoni mwa wiki iliyopita kujadili uteuzi wa meneja wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino ili awe meneja ajaye wa klabu hiyo ya Stamford Bridge. (Evening Standard)
Mmiliki wa Arsenal Stan Kroenke anatarajiwa kumpa meneja wa Gunners Mikel Arteta kitita cha pauni milioni 200 ili kuimarisha kikosi chake msimu wa joto. (Football transfers)
West Ham wameanza kutafuta kiungo mbadala wakijiandaa kumkosa mchezaji wa kimataifa wa England Declan Rice, 24 anayesakwa na Arsenal. (Football Insider)
Tottenham wanatarajiwa kupigana vikumbo na mahasimu wao wa London Kaskazini Arsenal katika mbio za kujaribu kumsajili beki wa Crystal Palace na England Marc Guehi, 22. (Evening Standard).
Bayern Munich wako tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya mshambuliaji wa Senegal Sadio Mane, 31, ambaye alijiunga nao akitokea Liverpool msimu uliopita wa joto. (90Min)
Fulham wanapanga kufanya mazungumzo na Leeds United kuhusu kumpa mkataba wa kudumu winga Muingereza Dan James, 25. (Football Insider)
BBC