Geita Gold yaipania Mbeya City

Joel JJ By Joel JJ β€’ 3rd May 2023


Geita Gold yaipania Mbeya City

Baada ya kupoteza mchezo wa ligi kuu uliopita dhidi ya Prisons katika uwanja wao wa Nyankumbu, Geita Gold imepania kurejesha wimbi la ushindi katika mchezo unaofuata dhidi ya Mbeya City

Kocha msaidizi wa Geita Gold, Mathias Wandiba amesema hawakufurahishwa na kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Prisons na kwamba makosa yaliyojitokeza hawatarajii kujirudia kwenye mechi zilizobaki na kwamba hasira zote ni kwa Mbeya City

"Kwa ujumla matokeo hayo yalituumiza sana, ila haijirudii kwa sasa tunajipanga upya na mchezo ujao dhidi ya Mbeya City tukihitaji ushindi ili kuendelea kulinda nafasi yetu,” alisema Wandiba

Alisema wanaamini kwa maandalizi waliyonayo hawapoteza mchezo wowote ili kufikia malengo akiwaomba mashabiki kuendelea kuisapoti timu hiyo hadi mwisho wa ligi

Mchezo kati ya Geita Gold dhidi ya Mbeya City utapigwa May 13 katika uwanja wa Nyankumbu, Geita


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.