Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi May 04 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
4 May 2023
Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi May 04 2023

Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 35, anaweza kumfuata hasimu wake Mreno Cristiano Ronaldo, 38, huko Saudi Arabia kwa uhamisho wa pauni milioni 320 kwa mwaka katika nchi ya Ghuba baada ya kuthibitisha kuwa anaondoka Paris St-Germain. (Telegraph)

Klabu ya Saudia ya Al-Hilal huenda ikaingia vitani kuwania saini ya Messi dhidi ya klabu ya Inter Miami inayoshiriki Ligi Kuu, inayomilikiwa na nyota wa zamani wa Manchester United na Uingereza David Beckham. (Guardian)

Real Madrid wako kwenye mazungumzo kuhusu kumnunua kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na England Jude Bellingham, 19, lakini klabu hiyo ya Ujerumani inasema bado haijapokea ofa kutoka kwa wababe hao wa Uhispania. (Sky Germany)

Sheikh Jassim ameachana na mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Brazil Neymar, 31, ikiwa atafaulu kuinunua Manchester United - badala yake analenga kusajili nyota watatu wa Ufaransa Kylian Mbappe, 24, wa Paris St-German, Kingsley Coman wa Bayern Munich, 26, na Eduardo Camavinga, 20 wa Real Madrid (Bild's Christian Falk)

Kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice, 24, mshambuliaji wa Bayer Leverkusen Mfaransa Moussa Diaby, 23, na nyota wa Crystal Palace Wilfried Zaha, 30, wa Ivory Coast na Muingereza Marc Guehi, 22, ni miongoni mwa wachezaji wanaosakwa na kocha wa Arsenal Mikel Arteta kwenye orodha ya wachezaji sita wa kisajiliwa katika dirisha la msimu wa joto. (Mail)

Tottenham wanamtaka kiungo wa kati wa zamani wa Liverpool na Hispania Xabi Alonso, 41, kuwa mrithi wa Antonio Conte baada ya matakwa ya mshahara ya Julian Nagelsmann kuwatoa Spurs katika mbio za kumpata Mjerumani huyo. (Metro)

Mshambuliaji wa Uholanzi Wout Weghorst ana nia ya kusalia Manchester United lakini Mashetani Wekundu bado hawajaanza mazungumzo na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 kuhusu kusalia Old Trafford wakati mkopo wake kutoka Burnley utakapoisha. (Telegraph)

Roma wanataka pauni milioni 35-40 kwa ajili ya mshambuliaji wa Uingereza Tammy Abraham, 25. Manchester United, Tottenham na Paris St-Germain zinatarajiwa kupigana vikumbo katika dirisha lijalo la msimu wa joto kusaka saini yake (Calciomercato)

Klabu ya Ligue 1 ya Marseille itajielekeza kumsajili mchezaji wa Crystal Palace ambaye anamaliza kandarasi yake mwishoni mwa msimu, Zaha ikiwa itafuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya. (FootMercato)

Newcastle inaweza kumnasa winga wa zamani wa Leeds Raphinha wa Barcelona na Brazil na kumrejesha Ligi Kuu England kwa uhamisho wa pauni milioni 70 (Sun)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
7h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
7h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
7h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
11h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
14h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
15h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
16h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
16h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
17h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
18h ago
READ MORE β†’