Geita - Local

Mambo magumu kwa Mpole DR Congo

Joel JJ By Joel JJ
β€’
4 May 2023
Mambo magumu kwa Mpole DR Congo

Haukuwa msimu mzuri kwa straika wa FC Lupopo, Mtanzania George Mpole kucheza Ligi Kuu ya Congo kama ilivyokuwa matarajio yake ya awali, kutokana na ligi hiyo kusimamishwa ghafla

Mpole ambaye alijiunga na FC Lupopo kupitia usajili wa dirisha dogo akitokea Geita Gold, amejikuta malengo yake yanakwama, baada ya kuambiwa na vingozi wao na ligi hiyo imefutwa na sasa wasubiri taarifa upya

Mshambuliaji huyo amesema kinachoendelea kwa sasa wanasubiri maelekezo ya viongozi wao, kisha ajiandae kurejea Tanzania hadi wakati mwingine na wataambiwa warudi kambini kwa ajili ya msimu mpya(2023/24).

"Matarajio yangu ya kucheza kwa mafanikio yameingia dosari, kwanza nimekuta timu inacheza michuano ya CAF, ambayo nisingeruhusiwa kucheza, hivyo muda mwingi nilikuwa jukwaani, ingawa nilikuwa nafanya mazoezi na timu:

"Wakati huo ligi ilikuwa imesimama kupisha michuano ya CAF, hatujakaa sawa Ligi Kuu inafutwa, nimegundua kwa nini wachezaji wengi wa Congo wanapenda kucheza nje na nchi yao, kwani huku nimeziona changamoto nyingi:

"Ndio maana siwezi kuzungumzia ushindani ama kutofautisha Ligi Kuu Bara na huku kwani bado sijaiona labda kwa wakati mwingine nitakapopata nafasi ya kucheza," alisema 

Ligi ya Congo ilikuwa inachezwa na timu 20 na kinara ni AS Vita na katika mechi 10 imeshinda tisa, sare moja na ina pointi 28, FC Lupopo anayoichezea Mpole, ipo nafasi ya pili, imecheza michezo tisa, imeshinda saba, sare moja, imefungwa moja ina pointi 22.

Timu ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo ni Maniema imecheza mechi nane, imeshinda sita, sare moja na imepoteza mmoja, ina pointi 19 na TP Mazembe yenye pointi 15 imecheza mechi tisa, imeshinda nne, sare tatu na imefungwa miwili na ipo nafasi ya nne.

Kuna uwezekano mkubwa Lupopo wakashiriki tena michuano ya kimataifa mwakani kutokana na nafasi yao waliyomalizia.

Mwanaspoti

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
9h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
10h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
14h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
17h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
18h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
18h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
19h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
19h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
20h ago
READ MORE β†’