Transfer - International

Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa May 05 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
5 May 2023
Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa May 05 2023

Wamiliki wa Newcastle United wanavutiwa na mshambuliaji wa Paris St-Germain na Brazil Neymar, 31, wakati wanatazamia kufanya usajili wa 'marquee' msimu huu wa joto. (90min)

Chelsea wanafikiriwa kuwa miongoni mwa vilabu vinavyotaka kumsajili fowadi wa Argentina Lionel Messi, 35, mkataba wake wa PSG utakapokamilika msimu huu wa joto. (football London)

Wolves wanaweza kuwapa Barcelona euro 30m (£26.3m) pamoja na kiungo wa kati wa Ureno Ruben Neves, 26, kwa kiungo wa kati wa Uhispania Ansu Fati, 20. (Relevo - in Spanish).

Barcelona wameelekeza nguvu zao katika kumsajili kiungo wa kati wa Morocco Sofyan Amrabat, 26, kutoka Fiorentina, jambo ambalo linaweza kuongeza matumaini ya Arsenal kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania Martin Zubimendi, 24, kutoka Real Sociedad. (AS – In Hispanic)

Manchester United wanapiga hatua nzuri katika mazungumzo kuhusu kandarasi mpya ya mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 25, kwa matumaini ya kumuunganisha na mshambuliaji wa Tottenham ya Uingereza Harry Kane, 29. (Telegraph - subscription required)

Arsenal na Aston Villa ni miongoni mwa klabu zinazomfuatilia winga wa Barcelona Mhispania Ferran Torres, 23. (Talksport)

Villa wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Juventus na Serbia Dusan Vlahovic, 23, pamoja na Torres. (Telegraph – Subscription required)

Brighton wana uhakika wa kumsaini kiungo wa kati wa zamani wa England James Milner, 37, msimu huu kandarasi yake itakapokamilika Liverpool, ambao wameongeza juhudi zao za kumnunua kiungo wa kati wa Argentina Alexis Mac Allister, 24, kutoka Seagulls. (Guardian)

Fulham itadai zaidi ya £50m msimu huu wa joto kwa kiungo wa kati wa Ureno Joao Palhinha, 27, ambaye analengwa na Liverpool na Bayern Munich. (Football Insider)

Newcastle United wako katika nafasi nzuri ya kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa Khephren Thuram, 22, kutoka Nice, ambaye atakuwa tayari kwa ofa ya pauni milioni 60 msimu huu. (Football Insider)

Meneja mtarajiwa wa Chelsea Mauricio Pochettino atampa Romelu Lukaku nafasi nyingine ya kujiimarisha katika klabu hiyo wakati mshambuliaji huyo wa Ubelgiji, 29, atakaporejea kutoka kwa mkopo Inter Milan. (Gazzetta dello Sport – In Itali)

Harvey Barnes anaweza kumfuata kiungo mwenzake wa kati wa England James Maddison kwa kuondoka Leicester msimu huu wa joto, huku Newcastle, Tottenham na Aston Villa zikifikiriwa kumfuatilia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Mail)

West Ham wana wasiwasi kuhusu kumpoteza kiungo wa kati wa Jamhuri ya Czech Tomas Soucek, 28, msimu huu wa joto, pamoja na nahodha wao na kiungo wa kati wa Uingereza Declan Rice, 24. (Football Insider)

Reiss Nelson amekataa pendekezo la kwanza la mkataba mpya lililotolewa na Arsenal, huku klabu nyingi nchini Uingereza na pia nje ya nchi zikitaka uhamisho wa bure kwa winga huyo wa Uingereza, 23. (Fabrizio Romano)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
9h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
10h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
14h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
17h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
18h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
18h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
19h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
20h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
20h ago
READ MORE β†’