Napoli wametwaa taji lao la kwanza la Serie A kwa miaka 33 baada ya kuwa na msimu mzuri na kupelekea kikosi cha Luciano Spalletti kupoteza mechi tatu pekee za ligi
Napoli imekuwa timu ya tatu ya Serie A kuwahi kutawazwa mabingwa wakiwa wamebakisha mechi tano - baada ya Inter Milan msimu wa 2007/08 na Juventus 2018/19 - huku wakimaliza kusubiri kwa miaka 33 kwa ubingwa Alhamisi usiku.
Kwa hisani ya pengo la pointi 15 kwa Lazio katika nafasi ya pili, Napoli ilihitaji pointi moja tu ugenini kwa Udinese na licha ya kuwa nyuma kwa dakika 39, bao la kusawazisha la Victor Osimhen kipindi cha pili lilitosha kwa sare ya 1-1
Osimhen amefikisha mabao 22 akiwa amefunga mabao mengi zaidi ya Serie A msimu huu kuliko mchezaji yeyote wa Kiafrika aliyewahi kufunga. Samuel Eto'o hapo awali alishikilia rekodi hiyo akiwa na Inter baada ya kufunga mara 21 msimu wa 2010-11 lakini Osimhen sasa ameiboresha zaidi
Ni mara ya tatu katika historia ya klabu hiyo kwa Napoli kutwaa taji la Serie A na wamefanya hivyo kwa mara ya kwanza tangu gwiji wa klabu hiyo Diego Maradona alipowaongoza kutwaa mataji mwaka 1987 na 1990