Azam - Simba - Local

Simba kuifuata Azam Fc Mtwara leo

Joel JJ By Joel JJ
β€’
5 May 2023
Simba kuifuata Azam Fc Mtwara leo

Msafara wa kikosi cha Simba unatarajiwa kuondoka Ruangwa leo kuelekea Mtwara kwa ajili ya mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Azam Fc

Mchezo huo utapigwa Jumapili, May 07 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona

Baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc, Simba iliweka kambi ya siku mbili Ruangwa mkoani Lindi

Mkakati wa Simba ni kuitafuta fainali ya kombe la FA, ili kuhakikisha msimu huu inatwaa angalau taji moja

Baada ya kupoteza matumaini kwenye ubingwa wa Ligi Kuu, Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira na benchi lake la ufundi wamepania kushinda taji la FA

Hata hivyo watalazimika kuifunga Azam Fc ambayo msimu huu imechukua alama nne mbele ya Simba katika mechi za Ligi

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
4h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
4h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
4h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
8h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
11h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
12h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
12h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
13h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
14h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
15h ago
READ MORE β†’