Yanga - Local

Yanga, Serikali kutoa elimu kuzuia magonjwa ya mlipuko

Joel JJ By Joel JJ
β€’
6 May 2023
Yanga, Serikali kutoa elimu kuzuia magonjwa ya mlipuko

Klabu ya Yanga jana iliingia kwenye ushirikiano na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Saalam, Ofisi ya Afya ya Mkoa na UNICEF TCO katika jitihada za kuongeza uelewa kuhusu kuzuia na kudhibiti magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu. Andre Mtine, Mtendaji Mkuu wa Yanga SC alisema hayo jana Mei 5, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari

"Tunafurahi kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa katika kampeni ya kuongeza uelewa juu ya magonjwa yote ya kuharisha ikiwa ni pamoja na mlipuko wa kipindupindu. Tunaahidi kusaidia serikali kushughulikia visababishi vyote vya magonjwa ya kuharisha na kutapika katika Jiji la Dar es Salaam," alisema Mtine

Dk Rashid Mfaume, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, amesema ushirikiano huo ni mfano wa jinsi ushirikiano kati ya wadau tofauti unavyoweza kusaidia jukumu muhimu katika kukabiliana na changamoto za afya ya umma

"Tunafurahi kushirikiana na Yanga tena, kwani ushirikiano wetu wa awali kwenye Uviko ulifana sana. Tunatumaini kufikia watu wengi iwezekanavyo, " alisema Dk Mfaume

Mkurugenzi wa Matawi wa Yanga, Haji Mfikirwa amesema kitendo cha serikali kuanzisha ushirikiano huo na kuwakabidhi kampeni hiyo ya kupambana na kipindupindu inaonesha ukubwa wa klabu hayo

"Nasi kupitia matawi yetu tutahamasisha wanachama wetu kusambaza elimu dhidi ya magonjwa yote ya mlipuko," alisema Mfikirwa.

More Stories

Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
3h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
7h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
7h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
8h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
9h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
9h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
10h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
10h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
1d ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
1d ago
READ MORE β†’