Real Madrid - Osasuna - International

Real Madrid yatwaa Copa del Rey

Joel JJ By Joel JJ
β€’
7 May 2023
Real Madrid yatwaa Copa del Rey

Real Madrid wameshinda taji lao la 20 la Copa del Rey baada ya mabao mawili ya Rodrygo kuwawezesha vijana wa Carlo Ancelotti kushinda 2-1 dhidi ya Osasuna kwenye fainali ya 2023

Mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 22 alifunga bao katika kila kipindi huko Estadio La Cartuja na kuihakikishia Real ushindi wa kwanza wa Copa del Rey tangu 2014

Mechi hiyo ilikuwa mara ya pili tu kwa Osasuna kufika fainali ya Copa del Rey, na mechi ya awali ya klabu hiyo ilikuja mwaka 2005

Real walikuwa mbele ndani ya dakika mbili shukrani kwa Rodrygo kabla ya Lucas Torro kusawazisha mchezo dakika ya 58 kwa mkwaju mdogo kutoka kwenye eneo la hatari

Rodrygo alifunga bao lake la pili na la Real usiku huo huku zikiwa zimesalia dakika 20 baada ya shuti la Toni Kroos kuangukia kwenye njia yake na kupata ushindi mnono kwa timu yake

Ushindi huo pia ulikuwa ushindi wa pili kwa Carlo Ancelotti, baada ya kuiongoza Real kufanikiwa Copa del Rey mnamo 2014 taji lake la kwanza kuu katika kilabu

Real Madrid wana nafasi ya kumaliza msimu na mataji mawili baada ya taji hilo. Wako hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabinbwa barani Ulaya wakitarajiwa kucheza dhidi ya Manchester City

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
7h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
7h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
7h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
11h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
14h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
15h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
16h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
16h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
17h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
18h ago
READ MORE β†’