Newcastle - PSG - International

Newcastle United kumsajili Neymar

Joel JJ By Joel JJ
β€’
7 May 2023
Newcastle United kumsajili Neymar

Imeelezwa kuwa Sehemu kubwa ya wenye hisa katika klabu ya Newcastle United wameonesha nia ya kumsajili Mshambuliaji kutoka Brazil na Paris Saint-Germain (PSG), Neymar da Silva Santos Júnior

Kundi la wamiliki wenye hisa nyingi (PIF) wanataka Newcastle kufanya usajili mkubwa katika kipindi hiki cha majira ya joto na wanaamini wanaenda kumaliza msimu katika nne bora na kufuzu kwa michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na kutumia faida hiyo

Uhamisho unaowezekana kwa Cristiano Ronaldo pia umejadiliwa na PIF na wana mawasiliano ya moja kwa moja na klabu yake ya sasa ya Al-Nassr, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 hafikiriwi na kocha wa Newcastle, Eddie Howe

Vyanzo vya habari vimedai kuwa licha ya nia ya kumtaka Ronaldo, kamwe hawatamlazimisha mchezaji yeyote katika kikosi cha kocha, ambacho yeye na benchi lake la ufundi hawana mpango naye

Hata hivyo, Neymar ni suala tofauti. Newcastle iko sokoni ikimsaka mshambuliaji wa kushoto kabla ya msimu ujao ili kuimarisha kikosi chao wakati wakijiandaa kurejea katika Ligi ya Mabingwa

Neymar mwenye umri wa miaka 31 anaonekana anafiti kabisa katika kikosi hicho, huku tayari kukiwa na muunganiko mzuri wa Wabrazil pamoja na Bruno Guimaraes na Joelinton wachezaji wawili maarufu sana katika timu hiyo msimu huu

PSG iko mbioni kumpiga bei Neymar katika kipindi cha majira ya joto, huku wengi wakifikiria kuwa kama ni uvunjifu wa tamaduni katika klabu hiyo, huku Lionel Messi akithibitishwa kuondoka baada ya kwenda Saudi Arabia bila ruhusa

Neymar amekuwa na PSG tangu mwaka 2017 wakati walipoilipa Barcelona kiasi cha Euro milioni 222, ambacho kilikuwa rekodi ya usajili kwa wakati huo

Vyanzo vimesema kuwa PSG inataka kiasi cha Pauni million 75 ili kumuachia mchezaji huyo. Manchester United, Manchester City na Chelse nao pia wamehusishwa na kutaka kumsajili mchezaji huyo

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
7h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
7h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
7h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
11h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
14h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
15h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
16h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
16h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
17h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
18h ago
READ MORE β†’