Azam - Simba - Local

Mgunda alia na kipigo Azam Fc

Joel JJ By Joel JJ
β€’
8 May 2023
Mgunda alia na kipigo Azam Fc

Kocha Msaidizi wa Simba Juma Mgunda amesema anatambua maumivu ambayo Wanasimba wanapitia baada ya kushuhudia timu yao ikitokewa hatua ya nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kwa kufungwa mabao 2-1 na Azam Fc katika mchezo uliopigwa jana uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara

Mgunda amesema matokeo hayo yamewaumiza hata wao katika benchi la ufundi, watajipanga na kufanya tathmini ya kilichotokea msimu huu ili kujipanga na kufanya vizuri zaidi msimu ujao

"Mimi naijua nguvu ya mashabiki uwanjani, ndio maana wanasema ni mchezaji wa 12, matokeo haya yamewaumiza sana lakini hata sisi benchi la ufundi tumeumia kwani halikuwa kusudio letu. Mtu wa kwanza ambaye anataka matokeo ya ushindi ni Kocha na benchi lake la ufundi"

"Inapotokea matokeo ya namna hii yanaumiza, niwaambie mashabiki wa Simba kwamba imetuumiza sote. Kikubwa ni kujipanga na kukaa chini kuangalia tulikosea wapi ili siku za mbeleni tuweze kufanya vizuri zaidi"

"Naweza kusema msimu huu haujawa mzuri kwetu lakini sisi benchi la ufundi tumeona, viongozi wa Simba wameona na hii ni taasisi kubwa, itachukua hatua kurekebisha mapungufu ili kuhakikisha msimu ujao tunafanya vizuri," alisema Mgunda

Baada ya kipigo cha Azam Fc, ni kama Simba imepoteza matumaini ya kushinda taji lolote msimu huu kwani wako nyuma kwa alama saba kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC huku zikiwa zimesalia mechi tatu tu

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
46m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’