Hazard kumaliza mkataba Real Madrid

Joel JJ By Joel JJ β€’ 8th May 2023


Hazard kumaliza mkataba Real Madrid

Eden Hazard amefichua kuwa hana nia ya kuondoka Real Madrid kabla ya mkataba wake kukamilika 2024

Hazard alikua mchezaji ghali zaidi wa Real Madrid alipojiunga na wababe hao wa La Liga kutoka Chelsea kwa ada ya pauni milioni 130 mwaka 2019

Lakini tangu kuwasili kwake katika mji mkuu wa Uhispania, Hazard amekuwa na wakati mgumu katika ubora na utimamu wa mwili na amekuwa kivuli cha mchezaji huyo aliyejizolea umaarufu mkubwa Stamford Bridge

Ameanza ligi mara moja tu msimu huu na alikuwa mbadala katika ushindi wa 2-1 wa Copa del Rey dhidi ya Osasuna Jumamosi jioni

Mbelgiji huyo anakubali kwamba msimu wake haukuwa mzuri lakini alithibitisha kuwa anapanga kumaliza kandarasi yake Santiago Bernabeu

"Umekuwa mwaka mgumu," Hazard mwenye umri wa miaka 32 aliiambia Cadena SER, kwenye Daily Mail

"Kusema kweli, ninapanga kusalia Real Madrid msimu ujao. Natarajia kubaki kwani nataka kusherehekea mwaka wa mwisho wa mkataba ambao nimebakisha"

"Nina uhusiano mzuri na klabu na wachezaji pia. Nataka kucheza, lakini najua ni ngumu sana. Lazima nifanye kazi na natumai naweza kucheza zaidi," alisema Hazard


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.