Tetesi za soka Ulaya, Jumanne May 09 2023

Joel JJ By Joel JJ β€’ 9th May 2023


Tetesi za soka Ulaya, Jumanne May 09 2023

Mshambulizi wa Argentina Lionel Messi, ambaye kandarasi yake na PSG inamalizika majira ya joto, bado hajafikia makubaliano ya kujiunga na klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 hatarajiwi kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wake hadi mwisho wa msimu wa Ufaransa. tarehe 3 Juni. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

Mshauri wa soka wa Paris St-Germain Luis Campos amezungumza na wakala wa Jose Mourinho kuhusu uwezekano wa kocha huyo wa Roma kujiunga na klabu hiyo ya Ufaransa msimu huu wa joto. (RMC Sport - kwa Kifaransa)

Chelsea wanatazamia kumtoa mshambuliaji wa Marekani Christian Pulisic, 24, mwishoni mwa msimu huu na wanaweza kumtumia kama chambo cha kuwashawishi mabingwa wa Italia Napoli kuwauzia mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 24. (Mail)

Barcelona wameweka bei inayotakiwa ya euro 80m (£70m) kwa winga wa Brazil Raphinha, huku Newcastle United na Chelsea zikitaka kumrejesha mchezaji huyo wa zamani wa Leeds United, 26, kwenye Ligi ya Premia. (Sport - kwa Kihispania)

Klabu ya Ujerumani Bayer Leverkusen imefufua nia yake ya kumnunua kiungo wa kati wa Arsenal Granit Xhaka, 30, baada ya kujaribu kumsajili kiungo huyo wa Uswizi msimu uliopita. (Mirror)

West Ham hawajavutiwa na mchezaji anayetumika kama sehemu ya ofa yoyote kwa kumpata kiungo wa kati wa Uingereza Declan Rice bali wanataka thamani yao ya pauni milioni 100 kufikiwa ikiwa watamruhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kuondoka msimu wa joto. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Marseille na Ufaransa Matteo Guendouzi, 24, ananyatiwa na West Ham kwani wanamwona mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal kama mbadala wa nahodha Rice. (Athletic Usajili unahitajika)

Mshambuliaji wa Ufaransa Randal Kolo Muani atagharimu angalau euro milioni 90 sawa na (£79m) kwa klabu yoyote inayotaka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, kulingana na mtendaji mkuu wa Eintracht Frankfurt Axel Hellmann. (90 Min)

Winga wa Crystal Palace Michael Olise, 21, anawavutia wababe wa Ligue 1 Paris St-Germain, ambao wako tayari kuwasilisha ofa ya kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa chini ya umri wa miaka 21 msimu wa joto. (Mail)

Aston Villa, Leeds United na West Ham wamehusishwa na mshambuliaji wa Lyon Mfaransa Moussa Dembele, 26, ambaye aliwahi kuzichezea Fulham na Celtic. (Birmingham Mail)

BBC


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.