Yanga - Local

Yanga yapania ushindi dhidi ya Marumo Gallants

Joel JJ By Joel JJ
β€’
9 May 2023
Yanga yapania ushindi dhidi ya Marumo Gallants

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema Marumo ni timu nzuri, wamejiandaa kukabiliana nao kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Nabi alisema watachuana na Marumo iliyotinga nusu fainali kombe la Shirikisho na sio Marumo inayoshikanafasi za chini kwenye ligi kuu ya Afrika Kusini

"Marumo ni timu nzuri, sisi tumejiandaa kucheza na timu iliyofika nusu fainali na sio nafasi yao kwenye msimamo wa ligi ya kwao"

Nabi amesema wanatambua hawawezi kufuzu fainali kwa dakika 90 za mchezo wa kwanza nyumbani hapo kesho, wamejiandaa kwa ajili ya kupambana kwa dakika 180 za mechi zote mbili

"Ni mechi inayohitaji akili na tahadhari kubwa sana. Tunacheza mechi ya kwanza nyumbani lakini tunatambua hatuwezi kufuzu kwa matokeo ya mchezo mmoja. Tutacheza huku tukifahamu tuna dakika 180 za kufuzu"

"Wachezaji wote wako tayari kwa mchezo, ari ya timu ni kubwa kila mchezaji akitamani kuwa sehemu ya mechi hiyo," alisema Nabi

Nabi amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo ili kuwaongezea wachezaji wao hamasa ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri

"Niwashukuru sana mashabiki wa Yanga kwa sapoti mliyotupa kutoka mwanzo mpaka leo, nawaomba kesho tuongeze kitu kimoja. Kesho tushangilie kwa dakika zote 90, hata katika nyakati timu haina mpira tusiwe kimya, tupambane kushangilia ili kuwapa nguvu wachezaji wetu. Hii mechi sio nyepesi kama wengi wanavyodhani"

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
9h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
10h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
14h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
17h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
18h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
18h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
19h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
20h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
20h ago
READ MORE β†’