Real Madrid, Manchester City zatoshana nguvu UEFA CL

Joel JJ By Joel JJ β€’ 10th May 2023


Real Madrid, Manchester City zatoshana nguvu UEFA CL

Zilikuwa dakika dakika 90 za kibabe kwenye uwanja wa Bernabeu, Real Madrid na Manchester City wanatoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa mkondo wa kwanza nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya

Ilikuwa ni mechi ya vipindi viwili. Manchester City walimiliki mpira mwingi zaidi katika kipindi cha kwanza. Kuanzia dakika ya kwanza, walishambulia zaidi, na kujaribu kuibana Real Madrid kwenye nusu yao. 

Hata hivyo ni Real Madrid waliotangulia kufunga kwenye dakika ya 36 kupitia kwa Vinicious Junior aliyepiga shuti kali nje ya 18 baada ya pasi kutoka kwa Eduardo Camavinga

Real Madrid ilikwenda mapumziko ikiwa na uongozi wa bao 1-0 na ikarejea kipindi cha pili ikiwa na kasi ileile wakisaka bao la ushindi

Manchester City wakajibu kwenye dakika ya 67 Calvin De Bruyne aliyekuwa nyota wa mchezo huo akaifungia bao akipiga shuti kutoka nje ya 18 kama alivyofanya Vini Jr

Sare hiyo inaufanya mchezo wa mkondo wa pili ambao utapigwa Etihad kuwa nafasi sawa kwa kila timu pamoja na kwamba City wanaweza kuwa na nafasi kubwa zaidi katika uwanja wa nyumbani

Hata hivyo msimu huu Real Madrid wamedhihirisha wanaweza kupata ushindi katika uwanja wowote iwe nyumbani au ugenini


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.