Simba kusukwa upya

Joel JJ By Joel JJ β€’ 10th May 2023


Simba kusukwa upya

Wakati msimu wa mashindano 2022/23 ukiwa unaelekea ukingoni, Mtendaji Mkuu wa Simba Imani Kajula amesema wanatarajia kufanya maboresho makubwa ya kikosi ili kuhakikisha msimu ujao Simba inaweza kutimiza malengo yake katika mashindano yote ambayo itashiriki

Msimu ujao Simba itashiriki Ligi Kuu, FA Cup, Ligi ya Mabingwa na Super Ligi inayotarajiwa kuanza mwezi Oktoba 2023

Imeelezwa tayari kocha mkuu wa Simba Robertinho Oliveira amewasilisha mapendekezo ya wachezaji ambao anawahitaji katika kikosi chake pamoja na orodha ya wachezaji ambao hawako katika mpango wake

Wachezaji ambao huenda wasiwe sehemu ya kikosi cha Simba msimu ujao ni pamoja na Joash Onyango, Nassoro Kapama, Habib Kyombo, Mohammed Ouattara, Jimmyson Mwanuke, na Augustine Okrah

Wengine ni Nelson Okwa, Ismail Sawadogo na Victor Akpan, huku Erasto Nyoni na Peter Banda wakiwa kwenye hatihati

Aidha chanzo kutoka ndani ya uongozi wa Simba kimedokeza wachezaji ambao wako kwenye mpango wa Simba ni pamoja na kiungo mshambuliaji wa Vipers Fc Milton Karisa

Wengine ni beki wa kati wa Rayon Sports ya Rwanda, Abdul Rwatubyaye, kiungo wa Geita Gold, Edmund John na kipa wa Vipers FC ya Uganda, Alfred Mudekereza

Robertinho ameuagiza uongozi wa Simba kukamilisha michakato ya usajili mapema ili timu itakapokwenda pre-season awe na wachezaji wote atakaowatumia msimu ujao


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.