Kipa wa Tottenham na Ufaransa Hugo Lloris, 36, ana ofa ya kucheza Saudi Arabia msimu ujao kwa mshahara ambao ni mara tatu ya ule anaopokea sasa katika klabu ya Spurs. (Times - usajili unahitajika)
Newcastle wamefufua nia yao ya kumnunua kiungo wa Leicester mwenye umri wa miaka 26 James Maddison. (Telegraph - usajili unahitajika)
Liverpool wana nia ya kumsajili kiungo wa Real Madrid na Ufaransa Aurelien Tchouameni, 23, walau kwa mkataba wa mkopo. (90 Min)
Tottenham wanamtafu atakayechukua nafasi ya mkurugenzi mkuu wa zamani Fabio Paratici kabla ya kukamilisha mipango ya kumsajili kocha mpya. (Mirror)
Manchester City wameelekeza darubini yao kwa kiungo wa kati wa Chelsea na Croatia Mateo Kovacic mwenye umri wa miaka 29 kama mbadala wa kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham, 19, ambaye anatazamiwa kujiunga na Real Madrid kutoka Borussia Dortmund. (Football Insider)
Liverpool wako tayari kumsajili mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani na klabu ya Hannover 96, Ron-Robert Zieler, 34 kama kipa wa ziada (Bild - kwa Kijerumani)
Napoli wameongeza bei ya Victor Osimhen hadi euro milioni 160 wakitarajia kinyang'anyiro kikali baina ya vilabu vinavyomwania mshambuliaji huyo wa Nigeria mwenye umri wa miaka 24. (Il Matino - kwa Kiitaliano)
Mshambulizi wa AC Milan na Ureno Rafael Leao, 23, ambaye amekuwa akihusishwa na Liverpool na Chelsea, amesaini mkataba mpya wa miaka mitano na klabu hiyo ya Italia. (Athletic- Usajili unahitajika)
Manchester United inamfuatilia mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, 25. (Football Insider)
Kipa wa Uingereza Aaron Ramsdale, 24, anakaribia kuafiki mkataba mpya wa muda mrefu Arsenal. (ESPN)
Sunderland wanapanga kumpa Jack Clarke kandarasi mpya ili kusambaratisha nia ya Crystal Palace na Brentford kumnunua mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 22. (TeamTalk)
Mshambuliaji wa Barcelona Mbrazil Raphinha, 26, ambaye amekuwa akihusishwa na Newcastle, amekanusha madai kuwa yuko tayari kuondoka Nou Camp msimu huu wa joto. (Chronicle Live)
BBC



