Inter Milan imepata ushindi muhimu wa mabao 2-0 dhidi ya mpinzani wake mkali AC Milan katika mchezo wa mkondo wa kwanza nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya (UEFA CL)
Mabao kutoka kwa Mkhitaryan na Dzeka yameisaidia Inter kupata ushindi unaowaweka katika nafasi nzuri ya kutinga fainali
Timu hizo zitarudiana tena wiki ijayo katika mchezo wa mkondo wa pili utakaopigwa hapo hapo kwenye uwanja wa San Siro
Ili kupindua matokeo AC Milan watahitaji ushindi wa kuanzia mabao matatu wakati Inter wao watahitaji sare au ushindi na hata wakipoteza kwa tofauti ya bao 1 watatinga fainali