Ijumaa May 12 Simba itashuka uwanja wa Azam Complex, Chamazi kuikabili Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Nahodha wa Simba John Bocco amesema dhamira yao ni kuhakikisha wanashinda mechi zote tatu zilizosalia wakianza na mchezo dhidi ya Ruvu Shooting
Baada ya Simba kuondoshwa katika michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), pia matumaini ya kushinda ubingwa wa Ligi Kuu ni kama hayapo lakini wachezaji wa timu hiyo wamesema lengo lao ni kuhakikisha wanatumia mechi zilizobaki kuwaomba radhi mashabiki wao
Wachezaji wote wa Simba walirejea mazoezini siku moja baada ya timu kutoka mkoani Mtwara na wote jana walishiriki mazoezi
Leo Simba itakamilisha maandalizi yake tayari kwa mchezo huo utakaopigwa majira ya saa 1 usiku



