Yanga - Local

Yanga yapania kutangaza ubingwa mbele ya Dodoma Jiji

Joel JJ By Joel JJ
β€’
12 May 2023
Yanga yapania kutangaza ubingwa mbele ya Dodoma Jiji

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema wanahitaji kupambana kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa uwanja wa Azam Complex hapo kesho ili kuhakikisha wanashinda na kutwaa ubingwa

Nabi amesema anawaheshimu Dodoma Jiji ni timu nzuri lakini muhimu kwa timu yake ni alama tatu ambazo zitawahakikishia ubingwa

"Tumetoka kucheza mchezo wa kwanza wa nusu fainali kombe la Shirikisho, yapo mapungufu tuliyaona katika mchezo huo ambayo tumeyafanyia kazi"

"Japo tuna changamoto ya uchovu na majeraha kwa baadhi ya wachezaji, lakini nina imani na wachezaji wangu wale watakaopata nafasi kesho watapambana kutupatia ushindi"

"Nawaheshimu Dodoma Jiji ni timu nzuri lakini sisi malengo yetu ni kutafuta ushindi ili tuweze kuwa mabingwa," alisema Nabi

Nae mshambuliaji kinara wa mabao Fiston Mayele amesema kwa upande wa wachezaji mawazo yao ni kushinda mchezo dhidi ya Dodoma Jiji ili wawe mabingwa

Akiwa kiongozi kwenye safu ya ushambuliaji, Mayele amewaahidi Wananchi kuwa kama atapewa nafasi ya kucheza mchezo huo, atapambana ili awape furaha

"Sisi wachezaji tuko tayari kwa mchezo dhidi ya Dodoma Jiji, tumeshasahau furaha ya ushindi wa juzi. Binafsi kama nitapewa nafasi ya kucheza hapo kesho nitahakikisha napambana ili niwape furaha mashabiki wa Yanga," alisema Mayele

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
9h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
10h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
14h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
17h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
18h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
18h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
19h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
20h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
20h ago
READ MORE β†’