Yanga - Local

Serikali yagharamia mashabiki 55 kuishangilia Yanga Afrika Kusini

Joel JJ By Joel JJ
β€’
14 May 2023
Serikali yagharamia mashabiki 55 kuishangilia Yanga Afrika Kusini

Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo katika juhudi za hamasa kuendelea kuunga mkono michezo nchini hususani katika mashindano ya kimataifa, imegharamia jumla ya mashabiki 55 watakaosafiri kuelekea nchini Afrika Kusini, kwenda kuishangilia klabu ya Yanga

Ni katika mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Marumo Gallants, utakaopigwa tarehe 17 Mei, 2023 kwenye uwanja wa Royal Bafokeng uliopo katika mji wa Rustenburg nchini humo

Hayo yalielezwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Saidi Yakubu alipokuwa anazungumza na vyombo vya habari jana Mei 13, katika ukumbi wa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam

Yakubu alisema msafara huo wa hamasa utaongozwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Hamis Mwinjuma

"Katika hii safari, Serikali imesaidia Yanga kupeleka baadhi ya mashabiki 55 ambao wataondoka kesho (leo) jumapili tarehe 14 Mei, 2023 kueleka Afrika Kusini na huko wataungana na Watanzania waishio Afrika Kusini katika kuhakikisha wanatoa hamasa ya kutosha"

"Nimeongea na Balozi, wao pia wamejiandaa kuwapokea lakini pia wameandaa mabasi kutoka kila mji kuhakikisha Watanzania wanakuwa wengi katika mchezo huo,"alisema Yakubu.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa klabu ya Yanga, Andrew Ntime alisema kuwa wao kama timu wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye mchezo huo huku akiishukuru serikali kutokana na mchango wake wa kupeleka mashabiki hao

Msafara wa Yanga umeondoka nchini Alfajiri ya leo Jumapili kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa Jumatano

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
3h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
4h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
5h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
6h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
6h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’