Tetesi za soka Ulaya, Jumapili May 14 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
14 May 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumapili May 14 2023

Meneja wa zamani wa Tottenham Hotspur na Paris St-Germain Mauricio Pochettino amekubali kuinoa Chelsea msimu huu wa joto. (Telegraph)

Pochettino anataka Mason Mount kusalia Stamford Bridge, ingawa kiungo huyo wa kati wa Uingereza mwenye umri wa miaka 24 amebakisha mwaka mmoja tu katika kandarasi yake na hajapewa nyongeza ya muda. (Mail)

Liverpool wako tayari kufikisha kileleni mbio za kumnunua mshindi wa Kombe la Dunia Alexis Mac Allister kwa dili la pauni milioni 70 kumnunua kiungo huyo wa kati wa Brighton na Argentina (Mirror)

Beki wa Manchester City na England Kyle Walker, 32, yuko tayari kukataa kutoka nje ya nchi na kukamilisha miezi 12 ya mwisho ya kandarasi yake katika uwanja wa Etihad. (Sun)

Beki wa Manchester United na Argentina Lisandro Martinez, 25, anatarajia kuongezwa mshahara msimu huu wa joto punde tu masuala ya umiliki wa klabu hiyo yatakapotatuliwa. (Sun)

Everton watakuwa tayari kukubali pauni milioni 50 msimu huu kwa mlinzi wa Ubelgiji Amadou Onana ikiwa watashushwa daraja kutoka Ligi ya Premia. (Football Insider)

Barcelona wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Wolves na Ureno Ruben Neves, 26. (Talksport)

Kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham aliripotiwa kukataa kuhama kutoka Borussia Dortmund kwenda Manchester City. (FourFourTwo)

Aston Villa wanamtaka kiungo wa kati wa Real Madrid na Uhispania Marco Asensio, 27, na mshambuliaji wa Barcelona wa Uhispania Ferran Torres, 23. (Sport - in Spanish)

Lakini Torres amesisitiza kuwa anataka kubaki Barcelona na hajawasiliana na Villa. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Manchester United wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Bayern Munich na Uholanzi Ryan Gravenberch, 20, msimu huu wa joto. (Football Insider)

Rais wa klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia, Fahad Bin Saad Bin Nafel, amekataa kutoa maoni yake kuhusu uvumi wa uhamisho wa mshambuliaji wa Paris St-Germain na Argentina Lionel Messi, 35. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

Beki wa Liverpool mwenye viwango vya juu Isaac Mabaya, 18, ametia saini mkataba mpya na klabu hiyo. (Liverpool Echo)

Atletico Madrid wako kwenye mazungumzo na Racing Club de Montevideo kuhusu uhamisho wa beki wa kati wa Uruguay Santiago Mourino, 21. (Marca - in Spanish)

Meneja wa Manchester United Erik ten Hag amesisitiza kuwa ubora wa mchezaji ambaye klabu hiyo ya Old Trafford inaweza kumsajili umeongezeka zaidi ya mwaka mmoja uliopita. (90 Min)

Manchester City wanakaribia kukamilisha dili la kumsajili mlinda mlango wa England Under-16 Spike Brits, 15, kutoka AFC Wimbledon. (Fabrizio Romano)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
7h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
9h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
9h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
10h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
10h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
11h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
14h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
16h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
17h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
17h ago
READ MORE β†’