Kitu pekee kinachowaumiza Wanasimba ni kuona wameshindwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu licha ya kuwa na kikosi bora sana msimu huu
Ukiangalia takwimu, Simba imeongoza katika kufunga na kutengeneza nafasi nyingi za mabao
Wachezaji Saido Ntibazonkiza na Clatous Chama wana nafasi kubwa katika kinyan'ganyiro cha tuzo ya mchezaji bora wa msimu huu
Saido ndiye mchezaji aliyehusika katika mabao mengi zaidi msimu huu akiwa na assist 12 na pia akifunga mabao 10 na jumla kuhusika katika mabao 22 akiwa na Simba na Geita Gold
Chama yeye ametoa assist 14 na kufunga mabao 4 na hivyo kuhusika katika mabao 18 akiwa sawa na mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele aliyefunga mabao 16 na kutoa assist 2
Ni wazi Saido na Chama wanaweza kuchuana katika kinyang'anyiro cha mchezaji bora wa msimu Saido akiwa na nafasi kubwa zaidi
Katika msimu huu Simba imefunga mabao 66 na kuruhusu mabao 15 wakiwa wamefunga mabao 10 zaidi ya watani zao Yanga waliofunga mabao 55 timu zote zikiruhusu mabao 15
Simba ndio timu pekee iliyofungwa mechi moja tu mpaka sasa msimu huu



