Ligi Kuu ya NBC inaelekea ukingoni ambapo jana mechi tatu za raundi ya 28 zilipigwa huku raundi hiyo ikihitimishwa leo kwa mchezo kati ya Polisi Tanzania dhidi ya Mtibwa Sugar
Katika mechi zilizopigwa Jumapili, Tanzania Prisons ilijiweka kwenye eneo salama katika msimamo w aligi baada ya kuichapa Kagera Sugar bao 1-0
Prisons walifikisha alama 34 na kupanda mpaka nafasi ya nane katika msimamo
Coastal Union nayo ikapata ushindi muhimu wa bao 1-0 dhidi ya Ihefu Fc na kufikisha alama 33 ikisogea mpaka nafasi ya 10
Wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani, Azam Fc wakakumbana na kipigo wasichokitarajia kutoka kwa Namungo Fc
Mabao ya Hassan Kabunda na Shiza Kichuya yalitosha kuizamisha Azam Fc ambayo hata hivyo imeendelea kusalia katika nafasi ya tatu alama mbili mbele ya Singida BS
Hatma ya kubaki ligi kuu iko mikononi mwa Polisi Tanzania leo wakihitaji ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar
Ili kuwa na nafasi ya angalau kucheza Play-off, Polisi Tanzania wanahitaji kushinda mechi zote tatu zilizobaki wakati Mtibwa Sugar nao wanahitaji ushindi ili waondoke kwenye eneo la play-off