Kiungo mshambuliaji wa Simba Pape Ousmane Sakho ameomba kuvunja mkataba na Wekundu hao wa Msimbazi, imefahamika
Wawakilishi wa mchezaji huyo wamedai kutoridhishwa na kukosekana kwa muda wa kucheza kwa mteja wao ndani ya Simba, wakiamini Msenegal huyo anastahili muda zaidi wa kucheza.
Kulingana na Mwanahabari jr_farhanjr, Wawakilishi wa Sakho wamewasilisha ofa kadhaa za mteja wao kwa Simba ambazo zitakuwa na maslahi kwa Simba kiuchumi ili Sakho aweze kuondoka kusaka changamoto mpya
Tayari Sakho ameandika barua ya kuvunja mkataba baada ya mechi dhidi ya Ruvu Shooting huku mkataba wake ukitaka alipe mshahara wa miezi mitatu tu ili mkataba uvunjike, mkataba wake ulikuwa miaka mitatu na ameshacheza miwili
Kumekuwa na taarifa kuwa nyota kadhaa wa klabu ya Simba wameomba kuruhusiwa kuondoka mwishoni mwa msimu. Beki Mkenya Joash Onyango ni miongoni mwa wachezaji hao