Man City yatinga fainali UEFA kibabe

Joel JJ By Joel JJ β€’ 18th May 2023


Man City yatinga fainali UEFA kibabe

Manchester City wametinga fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya kibabe wakiifumua Real Madrid 4-0 katika mchezo wao wa mkondo wa pili wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Uwanja wa Etihad

Bernardo Silva alifunga mabao mawili na kukiweka kikosi cha Pep Guardiola kudhibiti kabla ya kujifunga kutoka kwa Eder Militao na bao la mwisho la Julian Alvarez kufanya matokeo ya jumla kuwa 5-1

Manchester City watachuana na Inter Milan kwenye fainali itakayofanyika Istanbul Juni 10

Mbele ya umati wa mashabiki waliojitokeza Etihad, Thibaut Courtois aliokoa hatari ya kwanza dakika ya 13 mpira wa kichwa wa Erling Haaland kufuatia krosi ya Jack Grealish

Courtois alikuwapo tena kumzuia Haaland katika dakika ya 22. Raia huyo wa Norway aliruka juu zaidi na kupiga kichwa lakini Courtois aliweza kuokoa hatari hiyo

Hata hivyo, kikosi cha Pep Guardiola kiliongoza dakika moja baadaye kwa hisani ya Bernardo Silva. Kevin De Bruyne alimsogezea Silva ndani kwa pasi na mshambuliaji huyo wa Ureno akaweka mpira kimiani

Toni Kroos alikaribia kusawazisha bao muda mfupi baadaye wakati juhudi zake kutoka mbali zilipogonga mwamba wa goli

Lakini Silva alikuwa tayari kufunga bao lake la pili na la City katika mchezo huo baada ya dakika 37

Juhudi za Ilkay Gundogan ziliokolewa na Courtois na Silva alikuwa tayari kupenyeza kichwa chake nyuma ya wavu

Ederson akafanya kazi  mapema katika kipindi cha pili alipoondoa mpira wa faulo wa David Alaba

City walikuja tena na kufanya matokeo kuwa 3-0 dakika 15 kabla ya mchezo kumalizika. Mpira wa adhabu wa De Bruyne ulikutana na Manuel Akanji na juhudi zake mpira ukamgomga Eder Militao na kuingia wavuni

Julian Alvarez aliweka barafu kwenye keki kwa bao dakika za lala salama na kufanya matokeo kuwa 4-0 usiku na kwa jumla ya 5-1. Phil Foden aliyetokea benchi alicheza pasi nzuri sana kwenye njia ya Alvarez ambaye alikuwa na utulivu, akamchambua Courtois


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.