Rais Dk Samia Suluhu ametangaza kuipa timu ya Yanga sh milioni 20 kwa kila goli itakayofunga kwenye mchezo wa fainali dhidi ya timu ya USM Alger itakayochezwa Mei 28, 2023 kwenye uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam na mchezo wa marudio utafanyika nchini Algeria Juni 3, 2023
"Wakati Simba na Yanga zinacheza nilisema kila goli sh milioni 5, Yanga iliposonga mbele nikasema Sh milioni 10 lakini sasa imefika fainali kila goli watakaloshinda nitatoa sh milioni 20," alisema Dk Samia
Aidha Rais Samia ameaidhi kutoa ndege kwa timu hiyo ya Jangwani itakapoenda kucheza mchezo wake wa marudiano
Yanga ilitinga fainali ya kombe la Shirikisho baada ya ushindi wa jumla wa mabao 4-1 dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini kwenye mechi za nusu fainali



