Klabu ya Simba tayari imeanza michakato ya maboresho ya kikosi kuelekea msimu wa 2023/24 ambapo inatajwa kumuwania winga wa Geita Gold, Edmund John
Kinda huyo mwenye umri wa miaka 20 anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wazawa waliomvutia kocha Robertinho Oliveira ambaye anahitaji kuongezewa mawinga
"Mazungumzo yanaendelea baina ya Simba na mchezaji na yanakaribioa kufikia pazuri. Tunafahamu ana mkataba na Geita Gold hadi Januari mwakani lakini tunaweza kuzungumza nao na tukafikia mwafaka wala hakuna shida katika hilo"
"Kocha amependekeza tusajili mawinga wawili wazawa ambao wataleta ushindani kwa wageni na huyu Edmund ni miongoni mwa wachezaji wa nafasi hiyo walioonyesha kiwango kizuri msimu huu," kigogo wa usajili Simba alinukuliwa na Mwanaspoti
Kama Simba itafanikiwa kumnasa Edmund atakuwa mchezaji wa pili kusajili na wekundu hao wa Msimbazi baada ya Saido Ntobazonkiza wote wakitokea Geita Gold