Real Madrid - International

Vini Jr awaponza marefa wa VAR La Liga

Joel JJ By Joel JJ
23 May 2023
Vini Jr awaponza marefa wa VAR La Liga

Shirikisho la Soka la Uhispania (RFEF) limewafuta kazi Waamuzi 6 wa VAR akiwemo Mwamuzi Ignacio Iglesias Villanueva ambaye alipendekeza Vinicius Junior kutolewa kwa kadi nyekundu katika mechi ya Valencia dhidi ya Real Madrid

Kwa mujibu wa vyombo vya Habari Nchini Uhispania, Shirikisho hilo halikufurahishwa na utendaji kazi wa Villanueva ambaye inadaiwa aliondoa picha iliyokuwa ikionesha mchezaji wa Valencia Hugo Duro akimkaba koo Vini Jr kwa nyuma

Villanueva alimwita mwamuzi wa kati, Ricardo de Burgos Bengoetxea kujiridhisha kwenye skrini ya VAR lakini VAR ilionyesha kipande kilichoonesha Vini Jr akimpiga Hugo usoni pekee huku kipande ambacho Duro akimkaba Vini Jr kwa nyuma kikiwa hakipo

Baada ya kujiridhisha Mwamuzi wa kati alitoa kadi nyekundu. Licha ya kuandamwa na kauli za matusi na ubaguzi wa rangi kwa kipindi chote cha mchezo Vinicius Junior alioneshwa kadi nyekundu lakini Duro ambaye alianzisha uchokozi aliendelea kusalia uwanjani

Vinicius Junior alikejeli kwa kupiga makofi baada ya uamuzi wa mwamuzi na baadae alirudia ishara iliyofanywa na Hugo Duro ya kukabwa kwa nyuma na kuhoji ukweli kwamba Duro hakuadhibiwa katika dimba la Mestalla ambapo Real Madrid ilipoteza 1-0 dhidi ya wenyeji Valencia siku ya Jumapili.

More Stories

Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
8h ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
9h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
11h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
11h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
12h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
12h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
13h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
13h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
13h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
15h ago
READ MORE →