Arsenal wako tayari kuuza wachezaji wanane wa kikosi cha kwanza msimu huu, huku kiungo wa kati wa Leicester City na Muingereza James Maddison, 26, na kiungo wa kati wa West Ham ya Uingereza Declan Rice, 24, wakiwa miongoni mwa wachezaji wapya wanaopania kuwasajili. (Mirror)
The Gunners wana nia ya kumnunua kiungo wa kati wa Ujerumani Ilkay Gundogan ikiwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 hatakubali mkataba kusaini mpya na Manchester City. (ESPN)
Real Madrid wamemuongeza nahodha wa Liverpool wa ScotlandAndy Robertson, 29, kwenye orodha ya wachezaji wanaoweza kuchukua nafasi ya beki wa Ufaransa Ferland Mendy, 27. (Mail)
Bayern Munich wamemtambua mshambuliaji wa Manchester City na Argentina Julian Alvarez, 23, kama mlengwa wa uhamisho wa majira ya joto. (Bild - kwa Kijerumani)
Manchester United wanafikiria kuwasajili washambuliaji wawili wapya wa safu ya kati - lakini wasiafikiane na Tottenham kuhusiana na usajili wa nahodha wa Uingereza Harry Kane, 29. (90min)
Mshambulizi wa Ajax Mghana Mohammed Kudus, ambaye amekuwa akihusishwa na Arsenal, Manchester United na Newcastle United, amekataa kuongezwa kwa mkataba katika klabu hiyo na wakala wake anaamini "sasa ni wakati mwafaka" kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kuondoka. (De Telegraaf - kwa Kiholanzi)
Everton wanapanga kumuuza kiungo wa kati wa Ubelgiji Amadou Onana, 21, kwa £60m ili kufadhili mipango yao ya uhamisho wa majira ya joto. (Football Insider)
Beki wa Ufaransa Jules Kounde ameiambia Barcelona kwamba anataka kuondoka katika klabu hiyo msimu wake wa joto, hata hivyo timu hiyo ya La Liga itazingatia tu ofa za euro 80m (£69.4m) kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Sport - kwa Kihispania)
Mshambulizi wa Ureno Cristiano Ronaldo tayari anataka kuondoka katika klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia na huenda akarejea Ulaya. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)
Juventus wamesema hawana nia ya kumuuza mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic mwenye umri wa miaka 23 baada ya kukatwa pointi katika hatua ambayo huenda ikaifanya klabu hiyo kukosa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa. (90 Min)
Klabu ya Uturuki Fenerbahce inaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji Divock Origi kutoka AC Milan, ambayo iko tayari kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 mwaka mmoja tu baada ya kujiunga kutoka Liverpool. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)
BBC



