Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumamosi May 27 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
27 May 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumamosi May 27 2023

Real Madrid wako tayari kutangaza hatua yao ya kusaini mkataba ya kiungo wa kati wa England Jude Bellingham, 19, kutoka Borussia Dortmund wiki ijayo. (Marca - in Spanish)

Kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice angependelea kujiunga na Arsenal msimu huu, huku Manchester United, Chelsea na Bayern Munich pia wakiwa na nia na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Mirror)

Manchester United bado hawakidhi kiwango cha Chelsea cha £55m ambayo ndio thamani waliyompa kiungo wa kati wa England Mason Mount licha ya kuongoza mbio za kinyang’anyiro cha kumchukua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka . (Independent)

Chelsea wanaangalia jinsi ya kumuuza mmoja wa walindalango wao wawili, huku mchezaji wa kimataifa wa Senegal Edouard Mendy, 31, akiwa na uwezekano mkubwa wa kuondoka katika klabu hiyo msimu huu . (90min)

Newcastle wamewatuma waangalizi wao kumfuatilia kwa karibu kiungo wa safu ya kati wa RB Leipzig na Hungary Dominik Szoboszlai, 22, mara mbili katika kipindi cha wiki mbili . (Sky Sports)

Manchester City wako tayari kutoka kitita cha euro milioni 40 (£35m) zinazohitajika kama garama ya kumnunua beki wa Ureno Joao Cancelo, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo katika Bayern Munich, huku Barcelona pia wakiwa na nia na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Sport - in Spanish)

City wanajiandaa kumtumia Cancelo katika mkataba wa kubadilishana wachezaji na kiungo wa kati wa Bayern na Ujerumani Joshua Kimmich, 28. (90min)

Marco Asensio yuko tayari kuondoka Real Madrid wakati mkataba wake utakapokamilika mwishoni mwa msimu huu baada ya mazungumzo baina ya klabu hiyo na kiungo huyo wa kati wa Uhispania mwenye umri wa miaka 27, kugonga mwamba. (Athletic - subscription required)

Asensio yuko katika mazungumzo ambayo yamefikia kiwango cha kukaribia kujiunga na Paris St-Germain kama wakala huru. (ESPN)

Tottenham wanaongoza katika mbio za kununua mlindalango wa Brentford na Uhispania David Raya, 27. (GiveMesport)

Mlindalango wa SC Freiburg na Netherlands Mark Flekken anakaribia kabisa kusaini mkataba kwa ajili ya kujiunga na Brentford, huku klabu hiyo ya Primia Ligi ikiwa tayari kurefusha mkataba na kijana huyo mwenye umri wa miaka 29-wenye kipengele cha thamani ya €13m (£10.4m) cha kumuachilia. (Sky Sports Germany)

Leeds United huenda wasisaini mkataba wa kudumu msimu huu na kiungo wa kati wa United States Weston McKennie, 24, wakati mkataba wake wa mkopo utakapoisha katika Juventus . (Calciomercato - in Italian)

West Ham wwanamtaka beki wa Arsenal Mreno Nuno Tavares, 23, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo katika klabu ya Marseille. (Record - in Portuguese)

Winga wa Arsenal mwenye umri wa miaka 23-Muingereza Reiss Nelson yuko tayari kuafiki mkataba wa muda mrefu na klabu hiyo. (Athletic - subscription required) Tottenham wako tayari kusikiliza ofa ya mlinzi wa Wales are willing to listen to offers mwenye umri wa miaka 30, Ben Davies msimu huu. (Football Insider)

BBC

More Stories

Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
48m ago
READ MORE β†’
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
11h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
11h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
11h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
15h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
18h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
19h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
19h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
20h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
21h ago
READ MORE β†’