Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumapili May 28 2023

Joel JJ By Joel JJ
28 May 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumapili May 28 2023

Meneja wa Manchester United Erik ten Hag anatarajia mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford kuongeza mkataba wake na klabu hiyo ya Old Trafford, huku mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ukikamilika mwishoni mwa msimu wa 2023-24. (Viaplay, viaManchester Evening News)

Real Madrid itamsajili kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham, 19, kutoka Borussia Dortmund kwa mkataba wa thamani ya pauni milioni 87 pamoja na nyongeza za pauni milioni 21. (Sunday Mirror)

Meneja mpya mtarajiwa wa Chelsea Mauricio Pochettino anataka kumtathmini mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, ambaye mkopo wake katika klabu ya Inter Milan kutoka the Blues unamalizika msimu huu wa joto, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 anataka kusalia katika klabu hiyo ya Italia. (La Gazzetta dello Sport - In Italian)

Liverpool wameomba kufahamishwa kuhusu hali ya kiungo wa Ureno, Ruben Neves, ambaye anaingia miezi 12 ya mwisho ya mkataba wake na Wolves na amekuwa akihusishwa sana na Barcelona. (Football Insider)

Aston Villa, Newcastle United, Tottenham na Roma wanaweza kumtazama mshambuliaji wa Wolves mwenye umri wa miaka 27 Hwang Hee-chan kwani klabu hiyo ya Midlands inaweza kulazimika kuuza wachezaji ili kutimiza sheria za masuala ya fedha (FFP). (Sunday mirror)

Tottenham wanatafuta kumsajili winga wa Israel Manor Solomon, ambaye amekuwa akiichezea Fulham, baada ya Fifa kusema kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 anaweza kuondoka Shakhtar Donetsk kwa uhamisho wa bure msimu huu wa joto. (Athletic)

Arsenal wanafikiria kumnunua beki wa kulia wa Ufaransa Sacha Boey, 22, anayechezea klabu ya Galatasaray ya Uturuki. SundayTelegraph)

Arsenal ilikataa kuweka kipengele cha kuachilia huru katika mkataba mpya wa winga wa Uingereza Bukayo Saka, 21 na badala yake wakampa mkataba mfupi kuliko ilivyotarajiwa, ambao utaendelea hadi 2027. (Mail on Sunday).

Burnley wanafuatilia hali ya kiungo mkabaji wa Liverpool Fabio Carvalho na wako tayari kuhama kwa mkopo wa kudumu au kwa mkopo kwa Mreno huyo mwenye umri wa miaka 20. (Football Insider)

Mshambuliaji wa Ubelgiji Divock Origi anatazamiwa kuondoka AC Milan na, wakati vilabu vya Uturuki vinamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, fowadi huyo wa zamani wa Liverpool angependelea kurejea katika Ligi ya Premia. (Il Corriere dello Sport)

Brighton wako kwenye mazungumzo ya kumsajili mlinda mlango Mmarekani Brian Schwake, 21, kutoka klabu ya Livingston ya Scotland huku mlinda mlango wa Uhispania Robert Sanchez, 25, akizingatia mustakabali wake na Seagulls. (Mail on Sunday)

Andoni Iraola, ambaye awali alikuwa analengwa na Leeds United, anatarajiwa kuacha nafasi yake kama kocha wa Rayo Vallecano. (Mundo Deportivo- in Spanish)

BBC

More Stories

Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
30m ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
1h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
3h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
3h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
4h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
4h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
5h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
5h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
5h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
7h ago
READ MORE →